Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wawili wa familia moja wafariki kwa kutumbukia shimoni

Shimo Laua.png Watoto wawili wa familia moja wafariki kwa kutumbukia shimoni

Wed, 24 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto wawili wa familia moja katika Mtaa wa Mindu mkoani Morogoro, wamefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye shimo linalodhaniwa kuwa ni la choo, tukio lililotokea Aprili 23, 2024 saa 12 jioni.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mkwajuni kata ya Mindu Manispaa ya Morogoro Juma Ahmed Bilali, amesema walipojaribu kuwaokoa, walikuta tayari wamekwisha fariki dunia kwa kunasa kwenye tope chini ya shimo hilo.

Watoto hao ni Neema Emmanuel (11) mwanafunzi wa darasa la nne na Glory Geitan (12) anayeosma darasa la tano.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Shaban Marugujo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema miili ya watoto hao tayari imetolewa katika shimo hilo na imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live