Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto watatu wafia mtoni Bariadi

Wafa Mtoni Watoto.png Watoto watatu wafia mtoni Bariadi

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto watatu kutoka Shule ya Msingi Itubukilo B, Kijiji cha Pugu, Kata ya Itubukilo Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu wamefariki dunia baada ya mkokoteni waliokuwa wakisafiria baada kuchota mchanga Mtoni kusombwa na maji ukiwa unavutwa na ng’ombe sita.

Waliofariki ni Maleki Legi (16), Isaka Njile (14) na Wille Njile ambao ni Watoto wa familia moja huku Watoto wawili wakinusurika.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya hiyo amefika katika eneo hilo na kujumuika na Wananchi ambapo pamoja na kuwapa pole Wafiwa amewaasa Wazazi juu ya umuhimu wa kuzingatia malezi ya Watoto hususani kipindi hiki cha mvua kubwa.

“Ndugu zangu Wanakijiji cha Pugu kwa niaba ya Serikali nimesikitishwa na kusononeshwa na tukio hili la kusikitisha na kusononesha limekatisha maisha ya Watot wetu hawa ambao walitakiwa kuwa nyumbani wakati huu wa msimu wa mvua”

“Poleni sana Wazazi, Ndugu na Wanakijiji wote, nawasihi sana tuwe makini katika malezi ya watoto hususani katika kipindi hiki cha mvua, ni jambo la kusikitisha kusikia Watoto hawa wadogo walipewa jukumu la kwenda Mtoni kuchota mchanga tena wakiwa na mkokoteni uliokuwa unavutwa na ng’ombe 6 tofauti na umri wao”

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Simiyu Inspector Faustine Mtitu amewataka Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari pindi wavukapo Mito na madimbwi kwani kumekuwa na maji mengi ambayo yanaweza kuleta maafa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live