Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto watatu familia moja wafariki kwa ajali ya moto

Watoto Watatu Familia Moja Wafariki Kwa Ajali Ya Moto Watoto watatu familia moja wafariki kwa ajali ya moto

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: Malunde

Watoto watatu wa familia moja ya Bwana Mathayo Samson katika mtaa wa Igomelo kata ya Malunga Manispaa ya Kahama wamefariki Dunia kufuatia ajali ya moto.

Tukio hilo limetokea leo Novemba 30, 2022 majira ya saa kumi na moja alfajiri ambapo moto uliunguza Nyumba ya Mathayo Samson na kusababisha vifo vya watu watatu wakiwemo wanafunzi wawili.

Akizungumzia ajali hiyo Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi ambaye ameeleza juu ya tukio hilo huku akithibitisha vifo vya watu watatu waliofariki katika ajali hiyo ya moto.

“Leo tarehe 30 mwezi wa 11 ilikuwa majira ya saa kumi na moja asubuhi katika mtaa wa Igomelo kata ya Malunga Manispaa ya Kahama Mkoa wa Shinyanga Nyumba ya ndugu Mathayo Samson anaumri wa miaka 39 na mfanyabiashara Nyumba yake iliwaka moto na madhara yaliyosababisha ni vifo vya watu watatu,"amesema Kamanda Magomi.

Waliofariki katika ajali hiyo ni Dotto Juma mwenye umri wa Miaka 33 mkulima, Samson Mathayo mwenye umri wa Miaka 13 mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi ST. Antony of Padua pamoja na Joseph Samson mwenye umri wa miaka 7 mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi ST. Antony of Padua.

Kamanda Magomi amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na jeshi la zimamoto na uokozi limefanikiwa kufika katika eneo la tukio na kwamba jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.

Chanzo: Malunde