Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wanne wa familia moja wafariki wakidaiwa kula mihogo yenye sumu

87565 Watoto%255Bic Watoto wanne wa familia moja wafariki wakidaiwa kula mihogo yenye sumu

Sat, 7 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Watoto wanne wa familia moja katika kitongoji cha Germani kijiji cha Machochwe Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara nchini Tanzania wamefariki duani wakidaiwa kula mihogo yenye sumu.

Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo usiku wa kuamkia leo Jumamosi Desemba 7, 2019 na kudai polisi na daktari wameenda eneo la tukio.

Ofisa mtendaji wa kata ya Machochwe, Yohana Ole amesema watoto hao ni wa familia ya Juma Mnanka ambao walichimba mihogo hiyo na kutafuna mibichi.

"Walichimba mihogo mibichi wakatafuna na kusababisha kifo chao, tutapata taarifa baada ya uchunguzi,” amesema.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi

 

Chanzo: mwananchi.co.tz