Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wanaokimbia vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kupatiwa bima ya afya

Fri, 31 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Watoto 20 wanaohifadhiwa katika Kituo cha Nyumba Salama Mugumu Wilayani Serengeti mkoa wa Mara kukabidhiwa vyeti vya bima ya afya.

Mwaka jana Naibu wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile alipotembelea kituo hicho kinachohifadhi watoto wanaokimbia ukeketaji aliahidi kulipia watoto 20 Bima ya afya.

Katibu tawala wilaya ya Serengeti Cosmas Qamara kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo Nurdin Babu leo Ijumaa Mei 31, 2019 ameambia Mwananchi Digital kuwa wanatarajia kukabidhi vyeti hivyo leo baada ya kutoka shuleni.

Mratibu wa Kituo hicho Melina Galibona amesema watoto hao kupata bima ya afya itawapunguzia gharama za matibabu walizokuwa wanatumia.

Hata hivyo, amesema watoto waliopata msaada ni 20 kati ya zaidi ya 40 hivyo ameomba wadau wajitokeze kuwasaidia watoto hao wanaokimbia vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Chanzo: mwananchi.co.tz