WATOTO wilayani Longido mkoani Arusha wamelalamikia vitendo viovu vinavyofanywa na wazazi wao ikiwemo ulevi uliopindukia na kusahau majukumu yao katika familia hali inayopelekea maisha hatarishi kwa watoto.
lsrael Kashuma mtoto kutokea kata ya Kitumbeine, amesema watoto wengi wakifugaji wakike hunyimwa haki ya elimu na kulazimishwa kuolewa na hata wale waliopata fursa ya kusoma hukatishwa ndoto zao kutokana na mimba za utotoni, huku watoto wakiume wakipewa kazi ya kuchunga mifugo.
"Si watoto wakike pekee ndio hunyimwa haki ya elimu, hata sisi tunapewa majukumu ya kuchunga mifugo, hivyo watoto wote wa kimaasai tunakosa haki ya elimu tunaomba serikali itusaidie kuwapa elimu wazazi wetu watambue umuhimu wa kutusomesha" amesema Kashuma.
Adela Samson mtoto kutoka kata ya Namanga amesema wazazi wa eneo hilo huwatelekeza, huwapiga na kuwafukuza watoto nyumbani kutokana na hali ngumu ya maisha, hivyo hupelekea watoto kuzurura mitaani na wakati mwingine kuingia kwenye matukio ya wizi.
"Watoto wengi tunaishi na mzazi mmoja mama anapenda kufanya kazi kwa wasomali hataki kujua huku nyumbani tunakula nini au tunaishije tunateseka kweli" alidai Adela.
Akielezea kwa masikitiko wazazi wanavyojihusisha na masuala ya ulevi,alisema wakinamama wakilewa huleta wanaume nyumbani na kuwaambia watoto walale chini ,huku vitendo viovyu vikiendelea ila kwa upande wa kina baba wao huo kila siku mwanamke mwingine,hivyo vitendo hivyo vinawaumiza watoto hao.
"Ukimuomba mzazi matumizi anakuambia nenda kafanye kazi update ela nikijiangalia Mimi ni mtoto mdogo nitafanya kazi gani nipate pesa,tunafanyiwa matukio ya kikatili kutokana na wazazi wetu wanavyokaa mbali kutulea na kituacha kuzurura mitaani" amesema Adela.
Lucy Ruben Mkazi wa Namanga amesema wanwake wengi mpakani hapo wamezalishwa na waume za watu na wengine wamezalishwa na wanaume kutoka nchi jirani ya Kenya,hivyo wanaume ndio wamekua chanzo Cha mazingira magumu kwa watoto kwani wanwake hudai kulemewa na majukumu.
"Pamoja na adha wanwake wanayopotia lakini ni waombe wasikate tamaa kulea watoto wao,wawatunze na kuwajali" amesema Lucy.
Kaimu Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Arusha Daniel Kasikiwe, amesema watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wanazidi kuongezeka mkoani humo kutokana na ukuaji wa mji, watoto 54,911 wanaishi katika mazingira hatarishi huku watoto 22,921 wakiwa wameunganishwa na huduma mbalimbali ikiwemo afya, elimu, malezi kupitia serikali na wadau.
Kwa upande wake Ofisa usatawi wa jamii wilaya ya Longido Atunagile Chisunga, amesema kata ya Namanga ni kata inayoongoza kwa matukio ya kikatili kwa watoto ikiwemo ulawiti ubakaji na kuterekezwa,pia watoto wanatumika kusafirisha madawa ya kulevyia aina ya Mirungi na Bangi,kwa kupeleka mirungi Arusha na kuleta bangi Namanga tuliweza kushirikiana na Jeshi la Polisi tukawabaini wachache.
"Watoto wengi Namanga wameterekezwa hivyo wanajilea wenyewe hata wakifanyiwa matukio ya Kikatili hawana pakusemea , wazazi wamewaterekeza wapo kwenye kufanya kazi,tuna mitaa Saba tumefanikiwa kupata watu wawili wawili kila mtaa kwa kuunda kamati za MTAKUWA watao tupa taarifa za Watoto" amesema Chisunga.
Sheria ya ustawi wa mtoto Namba 21 ya mwaka 2009 imelenga kuimarisha ulinzi ,matunzo na haki za watoto Tanzania bara ,Sheria hii imeainisha haki ya mtoto kulelewa na wazazi,haki ya kupewa jina kuwa na utaifa, haki ya kupata mahitaji ya msingi Kama chakula, Malazi, Mavazi, Matibabu, Chanjo, Elimu pamoja na haki ya kucheza na kuburudika, na Sheria hii inasisitiza kuwa ni kinyume na Sheria kufanya vitendo vya ubaguzi, unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto.