Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wafariki kwa kulipukiwa na kitu kinachodhaniwa bomu

Screenshot 2021 05 29 At 11.45.46 660x400.png Watoto wafariki kwa kulipukiwa na kitu kinachodhaniwa bomu

Sat, 29 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Watoto wawili wamepoteza maisha baada ya kulipukiwa na kitu kinachodaiwa kuwa bomu katika kijiji cha Mugera, Kata ya Nyantakara wilayani Biharamulo mkoani Kagera.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi, amesema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 27 mwaka huu kati ya saa 12:00 na saa 1:00 jioni, na kutaja majina ya watoto waliopoteza maisha kuwa ni Daniel Joseph mwenye umri wa miaka 14 na Charles Njola mwenye umri wa miaka 16.

Kamanda Malimi amesema kuwa watoto hao waliokuwa wakijiandaa kurejea nyumbani kutoka eneo walilokwenda kuchunga ng’ombe waliokota chuma ambacho kinadhaniwa kuwa ni bomu na bila kujua walianza kukichezea na kusabababisha kulipuka na kuwachana sehemu mbalimbali za miili yao.

Chanzo: millardayo.com