Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wa kike 129 wafanyiwa ukatili Kasulu

Watt Kasulu Watoto wa kike 129 wafanyiwa ukatili Kasulu

Tue, 12 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Jumla ya watoto wa kike 129 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu wamefanyiwa ukatili wa aina mbalimbali kwa mwaka 2020/21 huku vitendo vya kubakwa na kutelekezwa kwa watoto vikishamiri.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, ambayo kiwilaya yamefanyika kata ya Makere ofisa maendeleo ya jamii, Subira Swai kwa niaba ya ofisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Victoria Makyao amesema katika wilaya hiyo matukio ya watoto wa kike kubakwa ni matukio 22 huku kutelekezwa yakiwa 75.

Amesema watoto hao wote waliofanyiwa ukatili wapo katika hatari ya kuacha shule, mimba za utotoni, magonjwa ya zinaa, vifo na kuwa na watoto wanaoongoza familia zao, ambapo ametaja makosa mengine ni pamoja na ndoa za utotoni 4.

“Ukatili wa kihisia 14, mimba za utotoni 8, usafirishwaji wa watoto 2 na ukatili wa kiuchumi 4, kwa hali yoyote ile jamii,wazazi,walezi na serikali pamoja na wadau tuna wajibu wa kushirikiana kuhakikisha tunapunguza vitendo vya ukatili vinavyosababishwa na uwepo wa maisha ya kidigitali,”amesema Makyao.

Awali akizungumza katika maadhimisho hayo, mratibu wa mradi wa Buhoma kutoka Shirika la World Vision Kasulu, Donasian Severine amesema ili kuweza kupunguza changamoto zinazoweza kumkumba mtoto wa kike kwenye maswala ya ukatili hasa kwa Tanzania ni kuwa na mjadala wa wazi kwasababu jambo hilo limekuwa endelevu kwa muda mrefu sana.

Amsema mjadala wa wazi utasaidia kulifanya jambo hilo kusikika na wengi ili liweze kuwekewa kwenye vipimo na vipaumbele vyao, kwa kuwaboreshea mazingira kwa kuwatengenezea mifumo bora ya elimu, afya na taasisi nyingine ambazo zitamfanya mtoto wa kike kuwa bize na kuweza kufikia ndoto zake.

Katika maadhimisho hayo, watoto wameiomba Serikali, wadau na wazazi kwa ujumla kuwapa ulinzi na kuwasimamia katika kuhakikisha wanafikia ndoto zao ikiwemo na kuboreshewa mazingira rafiki ya upatikanaji wa elimu.

“Tunaomba wazazi wapewe elimu ya kuwza kutulea watoto ili tuweze kufikia malengo yetu kwani kuna baadhi ya wazazi wamekuwa ni chanzo cha ukatili kwa kutuozesha mapema ili waweze kuapata fedha kwa tamaa zao,”amesema mwananfunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Makere Christina Boniface.

Mtoto Hanifa Mohamed amesema ni wakati sasa Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuona umuhimu wa wanafunzi kufundishwa elimu ya ukatili na jinsi ya kukabiliana na vitendo hivyo hasa kwa watoto wa kike ili aweze kujitambua na hatimaye kufikia malengo yake.

Chanzo: mwananchidigital