Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wa chekechea waangukiwa na ukuta shuleni, kadhaa wahofiwa kufa

50cc1495f48850165f1a5adc20511803 Watoto wa chekechea waangukiwa na ukuta shuleni, kadhaa wahofiwa kufa

Thu, 19 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Watoto watatu wanahofiwa kufariki dunia papo hapo leo asubuhi, Novemba 18, 2020, baada ya ukuta wa nyumba ya jirani kuiangukia Shule ya Chekechea ‘Joy Unit Nusery’ iliyopo kata ya Bonyoka Kisiwani, mtaa wa Zahanati, Tabata jijini Dar es salaam.

Mwandishi wa Daily News Digital, Tagato James Tagato alifika eneo la tukio na kukuta maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.

Taarifa za awali zilizotolewa na Afisa Mtendaji wa kata hiyo, Sunday Felician alipokuwa akizungumza na maafisa wa Jeshi hilo, waliofika eneo la tukio aliwaeleza kuwa, watoto watatu wanahofiwa kufariki na wengine wanne wamejeruhiwa.

Bofya hapa kutazama video BALAA SHULENI: Ukuta waangukia watoto wa chekechea Dar, kadhaa wahofiwa kufa

Chanzo: habarileo.co.tz