Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto kituo cha yatima Dar ‘kuiona’ Krismasi

Mon, 24 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Sikukuu ya Krimasi ikiadhimishwa kesho, watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Kind Heart Africa jijini hapa wana kila sababu ya kufurahi baada ya dhehebu la Budha kuwapatia msaada wa vyakula, nguo na vifaa vya shule.

Kwa mujibu wa waumini wa dhehebu hilo wenye asili ya Kichina, lengo la kutoa misaada hiyo ni kuwafanya watoto hao wajisikie na wao ni kama wengine ambao wana wazazi walio hai.

Akizungumza jijini hapa juzi, Masta wa jumuiya ya Lonquan Tanhua Monastery, Xian Ding alisema wametoa msaada huo kwa kushirikiana na kampuni ya Clean Nature ambayo inajihusisha na biashara ya nguo nchini.

“Sisi huwa tunaomba kampuni za Kichina zenye moyo wa kusaidia kuleta misaada yao kwa ajili ya watoto yatima. Ujio wa misaada hii ni matunda yetu na tutaendelea kuongea na wengine kadri tutakavyoweza,” alisema.

Aidha, Ding aliwataka watoto hao kusoma kwa bidii kwani elimu ndiyo msingi wa maisha yao ili siku za badaye waweze kusaidia wengine.

Naye mmiliki wa kampuni ya Clean Nature, Jimmy Chen alisema kwamba kampuni yake inaangalia uwezekano wa kufungua kiwanda cha kutengeneza nguo nchini.

Kwa upande wake, Ofisa Ustawi wa Jamii, Lucy Chamwi alisema kituo hicho kina watoto 103 ila 90 tu ndio wanaoishi kituoni wengine wapo vyuoni wanakosomea mambo mbalimbali.



Chanzo: mwananchi.co.tz