Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto 505,840 kupatiwa kingatiba Kigoma

Sudan Kuidhinisha Kampeni Ya Chanjo Dhidi Ya Surua Watoto 505,840 kupatiwa kingatiba Kigoma

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Afya kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI inaendesha zoezi la umezeshaji vidonge vya kingatiba kwa ajili ya kudhibiti magonjwa ya minyoo ya tumbo na Kichocho kwa watoto kuanzia miaka mitano hadi 14 katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Magharibi ikiwemo Mkoa wa Kigoma.

Akitoa Taarifa kwa Umma kuhusu zoezi hilo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa, Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Albert Msovela amesema mkoa umepokea vidonge 793,000 aina ya Plaziquantel na 548,200 Albendazole kwa lengo la kuchanja watoto 505,840 walioko ndani na nje ya utaratibu wa shule.

Amesema Wizara Afya kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele, imedhamiria kutekeleza mpango huo ili kuhakikisha watanzania wanakuwa na afya bora kwa kuwakinga dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika.

Amesisitiza kuwa ili malengo ya serikali yaweze kufikiwa, jamii inapaswa kutoa ushirikiano kwa wataalam wa afya katika kuwatambua walengwa na kuhakikisha wanafikiwa kisha kupatiwa huduma.

"Nitoe wito kwa wadau mbalimbali na jamii kwa ujumla kuhakikisha tunashirikiana na serikali katika utekelezaji wa zoezi hili ili walengwa wote waweze kufikiwa, aidha jamii iendelee kukumbuka wajibu wake katika kuhakikisha watoto wanapata chanjo mbalimbali kuendana na miongozo ya Sekta ya Afya" amesisitiza Msovela.

Zoezi la ugawaji kinga tiba ya magonjwa ya minyoo ya tumbo na Kichocho limeanza kutekelezwa kuanzia Novemba 13 hadi 25 Desemba 2023 likihusisha halmashauri nane za Mkoa wa Kigoma. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live