Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto 46 wazaliwa mkesha wa mwaka mpya Arusha, Manyara

34410 Pic+watoto Tanzania Web Photo

Tue, 1 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Manyara/Arusha.  Watoto 46 wamezaliwa katika mkesha wa mwaka 2019 mkoani Manyara na Arusha.

Akizungumza na Mwananchi leo Januari Mosi, 2019 mganga  mfawidhi mkoani Manyara, Dk Charles Mtabho amesema watoto 15 wamezaliwa kwenye hospitali ya mji wa Babati Mrara na wanne wamezaliwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa huo.

Naye kaimu mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Haydom mkoani humo,  Dk Paschal Mdoe amesema watoto wanane wamezaliwa kwenye mkesha wa mwaka mpya hospitalini hapo na kati yao, watatu wa kiume na watano wa kike.

Mganga wa kituo cha afya Mirerani,  Dk Emmanuel Mushi amesema watoto wawili wa kike na wa kiume wamezaliwa kwenye mkesha huo katika kituo hicho cha afya.

Mkoani Arusha watoto 10 wamezaliwa katika mkesha wa mwaka mpya katika hospitali ya Mkoa wa Arusha, huku wa kiume wakiwa wanane na wa kike wawili.

Muuguzi wa zamu, Shubila Mjwahuzi amesema wazazi na watoto wote wapo katika hali nzuri na wataruhusiwa wakati wowote kulingana na hali ya kila mmoja.

Katika hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Meru watoto saba walizaliwa, kati yao wa kiume wanne na wa kike watatu.



Chanzo: mwananchi.co.tz