Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mwanaidi Khamisi amesikitishwa na kitendo cha wilaya ya Tunduru iliyopo mkoa wa Ruvuma kuwepo na idadi kubwa ya mimba za utotoni ambapo kwa mwaka wa 2020/2021 watoto 343 wamepata mimba za utotoni katika wilaya hiyo na k
Akiongea na wananchi wa wilayani Tunduru jana Agosti 16 , Mwanaidi amewataka wazazi kukaa na watoto zao na kuwaelimisha ili waweze kuepeukana na vishawishi wanavyokumbana navyo katika maeoneo tofauti hususan wakiwa mashuleni.
“Watoto 343 kupata mimba za utotoni na kuacha masomo yao ni kubwa sana hii ni wilaya tu tukija kwenye mkoa sijui tutakuwa na idadi ya watoto wa ngapi tutakuwa hatuna viongozi bora katika nchi yetu kwa hiyo akina mama tujitahidi kukaa na watoto wetu kuwaeleza yale ambayo hayastahiki na kuondoka na ushawishi wanaoupata wakiwa katika safari zao za kwenda shule,” amesema Mwanaidi.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Dk. Julius Ningu amesema kuwa wao kama wilaya watafanya tathimini ili waweze kujua wapi wafanye marekebisho ili kuondoa changamoto hiyo.
Nao baadhi ya wazazi wameeleza kusikitishwa na kuwepo na idadi kubwa ya mimba za utotoni na kukubali kuwa tatizo hilo linaanzia kwao kwani hawako karibu na watoto wao hivyo wamesema watashirikiana na serikali ili kuondoa tatizo hilo.