Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto 32 darasa la awali waugua kwa kula matunda yenye sumu

Wanafunzi 2 Picvvb Watoto 32 darasa la awali waugua kwa kula matunda yenye sumu

Wed, 15 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto 32 wa Shule ya Msingi Mkomo wamekula matunda yanayodaiwa kuwa na sumu na kuzua taharuki shuleni hapo.

Akizungumza na Mwananchi shuleni hapo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mkomo, Bakari Likuani alisema kuwa ili kuwa ni muda wa mapumziko baada ya kengele kulia ikiwataka watoke nje wakanywe uji ndipo waliposhambulia matunda hayo.

“Baada ya dakika 30 kula matunda hayo, mtoto mmoja alianza kutapika mwalimu alihisi anaumwa, akamruhusu arudi nyumbani lakini aliporudi darasani alikuta darasa zima linatapika jambo ambalo lilimshtua na akamrudisha yule mtoto na kutoa huduma ya kwanza kwa kuwatapisha,” alisema Mwalimu Likuani.

Naye Zainabu Issa mzazi wa mtoto aliyekula matunda sumu, alisema kuwa shida ilijitokeza kwa aliyeleta taarifa alisema watoto wetu wamekula sumu.

“Unajua aliyeleta taarifa alituchanganya kwakuwa alisema watoto wetu wamekula sumu jambo ambalo lilizua taharuki. Hali hii haijawahi kujitokeza ingawa ilituchanganya sana, hebu fikiria unafika shuleni halafu watoto 32 uwakute wamelegea wote wanatapika,” amesema.

Naye Dadi Rutavi mkazi wa Kijiji cha Mkomo, Kata ya Chawi Halmashauri ya Mji Nanyamba alisema kuwa hawa ni watoto wadogo tukio hilo lilitushua.

“Tulioonyeshwa mti huo hatua ya kwanza tuliukata na kuuondoa kabisa katika eneo na hii itakuwa kampeni kwetu kila tunaukuta popote mtu huo tunauondoa kwakuwa umeshakuwa adui wa watoto wetu,” amesema.

“Hii taarifa ilikuwa kali na ya kusisimua, kwa wazazi hebu fikiria mzazi umekaa unajua mtoto yuko shuleni anasoma lakini sasa unaambiwa amekula sumu hali yake sio nzuri inashtua sana,” amesema.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi Msaidizi wa Zahanati ya Chawi, Kandidusi Fussi alisema kuwa alipokea watoto 32 wenye umri kati ya miaka 5-6 wa darasa la awali kutoka Shule ya Msingi Mkomo wanaodaiwa kula matunda yenye sumu.

“Watoto walikuwa na hali mbaya walilegea na kutapika ambapo tulitoa huduma ya kwanza kwakuwapa maziwa baada ya hapo wote walitapika na baadaye walirejea katika hali zao za awali tuliwaruhusu kwenda nyumbani,” alisema Fussi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live