Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto 1600 wafelishwa kukwepa gharama Muheza

Muheza Pic Watoto 1600 wafelishwa kukwepa gharama Muheza

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: mwanachidigital

Mbunge wa Viti Maalumu Husna Sekiboko (CCM) amedai kuwa kuna watoto 1,600 katika Tarafa ya Mlola wilaya ya Lushoto ambao walilazimishwa na wazazi wao kufanya vibaya kwenye mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.

Sekiboko ametaja sababu za kufanya hivyo kuwa ni gharama kubwa ambazo wanapitia wazazi katika kuwasomesha shule za Sekondari mbali na maeneo wanayoishi.

Ametoa taarifa hiyo jana Jumanne April 18, 2023 wakati akichangia kwenye hotuba ya Wizara ya Tamisemi ambapo amesema kuna watoto wanalazimika kutembea zaidi ya kilomita 10 kufuata shule ya kata.

“Mheshimiwa Spika, hili ni tatizo kubwa, wazazi wanawaambia watoto wao wasifanye vizuri kwenye mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi kwa sababu mtoto anasoma kwa gharama ya kati ya Sh600, 000 hadi Sh1 milioni kwa mwaka, hii ni gharama kubwa sana,” amesema Sekiboko.

Mbunge huyo amesema kuna madarasa zaidi ya 40 ambayo hayana wanafunzi jambao ambalo linaitia hasara Serikali ya zaidi ya Sh800 milioni wakati ungekuwa na utaratibu w akujenga mabweni na watoto wangesoma karibu.

Katika hatua nyingine mbunge huyo amezungumzia maagizo yanayotolewa na Tamisemi kwa walimu kwamba yanawachanganya walimu kwenye ufundishaji.

Amesema Tamisemi inapaswa kuacha mpango huo kwani kwenye taaluma wanapaswa waagize watu wa Wizara ya Elimu ili wao wajihusishe na mambo ya ujenzi na miundombinu pakee.

Hata hivyo amesema kitendo hicho kinawafanya walimu kuwa na mgomo wa chinichini kwa kuona kama wanaingiliwa kwenye taaluma wakatyi wanaotoa maagizo hawahusiki na taaluma.

Chanzo: mwanachidigital