Ripoti kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Alfred Mwakalebela, imeeleza idadi hiyo ni wastani wa Watoto 2 hadi 3 kwa Wiki ambao hufanyiwa Ukatili wa Kubakwa na Kulawitiwa.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kihesa Kilolo, Omary Juma, amesema Watoto 30 walibakwa na Kesi ziko Mahakamani lakini bado wanashindwa kudhibiti tatizo kwa sababu familia za Waathirika hazitoi ushirikiano kwa Vyombo vinavyofuatilia.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN) kuhusu hali ya Kimataifa ya Kuzuia Ukatili dhidi ya Watoto ya Mwaka 2020 ilionesha nusu ya Watoto Duniani (Takribani Watoto Bilioni 1) wanaathirika na Ukatili wa Kimwili, Kingono, Kisaikolojia na Kujeruhiwa.