Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto 10 waliopotea mkoani Mtwara wasakwa

Watoto 10 waliopotea mkoani Mtwara wasakwa

Fri, 1 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuwatafuta watoto 10 wanaodaiwa kupotea katika kijiji cha Mtimbwilimbwi mkoani humo.

Amewataka wenye taarifa kuhusu kupotea kwa watoto hao kutoa ushirikiano.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Oktoba 30, 2019 Mmanda amesema watoto wanaodaiwa kutoweka ni wanafunzi wenye umri kati ya miaka 10 hadi 16.

Amesema taarifa za kupotea kwao zilianza kusambaa Oktoba 26, 2019 baada ya mzazi mmoja kudai mwanaye haonekani, wazazi wengine kuanza kujitokeza.

“Hao watoto hawaonekani majumbani mwao, ilianza taratibu na baadaye idadi yao ikafika 10. Sasa hivi ni msimu wa korosho kuna vibarua wa kuokota korosho hivyo tunafuatilia na tumeshatoa maelezo.”

“Kama kuna mtu atamuona mtoto anafanya kibarua aangalie isije kuwa ndio hawa wanaotafutwa. Pia  hatutaacha kuwa na mashaka katika msimu huu wa korosho wenye pesa wanajifanya waganga wa tiba mbadala na wao wanaona kama fursa,” amesema Mmanda Ameongeza, “hakuna taarifa kuwa waliondoka kama kundi bali ni mzazi mmoja mmoja kusema hamuoni mwanaye ndio tukajikuta tuna hii idadi, sio kwamba labda walienda shule wakabebwa kama kundi hapana.”

Amesema ripoti za watoto hao kuanza kupotea zilianza kutolewa Oktoba 16 na kushika kasi kuanzia Oktoba 26.

Chanzo: mwananchi.co.tz