Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto 1,000 kupewa elimu ya usalama barabarani Mtwara

Barabara Iusalama.png Watoto 1,000 kupewa elimu ya usalama barabarani Mtwara

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya Watanzania 11,000 nchini wametajwa kupata ajali za barabarani kutokana na matukio mbalimbali huku vifo vingi vya watoto chini ya miaka 5; na vijana wenye umri wa miaka 29, vikihusishwa katika ajali hizo.

Akizungumza wakati wa kutoa elimu katika shule za msingi mkoani Mtwara, Mratibu wa Usalama Barabarani kwa Kanda ya Kusini Mashariki, Nassoro Mansour (Babulolo), amesema kuwa kila mwaka dunia inapoteza zaidi ya watu milioni 1.3 kutokana na ajali za barabarani.

Aidha Mansour amesema, ajali hizo pia huacha majeruhi zaidi ya milioni 50; ambapo kwa mujibu wa Jeshi la Polisi nchini, zaidi ya watu 11,000 wanapoteza maisha katika ajali hizo.

Kwa mantinki hiyo, Mratibu huyo amesema kuwa Mabalozi wa Usalama Barabarani, wanatarajia kuadhimisha wiki ya usalama barabarani kitaifa mkoani Mtwara, kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa elimu kwa wanafunzi, ili waweze kuzifahamu sheria na alama za barabarani.

“Elimu itakayotolewa itawezesha jamii yetu kufahamu hatari kubwa zilizopo barabarani...tunaamini kuwa itakuwa chachu ya kupunguza ajali hizo barabarani...kwa kuwapa elimu na kutoa nafasi ya kujifunza kwa vitendo kunaipunguzia Serikali mzigo mkubwa wa gharama za matibabu,” amesema Nassoro.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Uelimishaji Mkoa wa Mtwara, Inspekta Salma Irigo, amesema kuwa zaidi ya shule 10 zitafikiwa na kupatiwa elimu ya masuala ya usalama wa barabarani.

“Tunatoa elimu kwa vitendo, tunawatembelea shuleni kisha tunaenda nao barabarani tukiwaelekeza sehemu sahihi ya kuvuka, na pia tutawaonyesha alama za barabarani, zikiwemo taa na matumizi yake na namna ya kuvuka na watoto wadogo,”

Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Msijute, Hamza Nambunga amesema kuwa wanafunzi wengi wanahitaji elimu ya masuala ya usalama barabarani kwakuwa wamekuwa wakitumia barabara bila kuwa na elimu wala tahadhari yoyote.

“Watoto wengi hawana elimu ya kuvuka barabara na wenigne wanaogopa zebra bila msaada hawavuki, hivyo mafunzo haya kwa vitendo yanaenda kusaidia watoto wetu ambao kimsingi ni wadogo, jambo ambalo limekuwa likisababisha ajali kuwa nyingi nchini,” amesema Nambunga.

Kwa Said Nawanda ambaye ni Mkazi kutoka eneo hilo la Msijute anaamini mafunzo hayo ni mazuri, hivyo ametpoa wito wa kuyafanya kuwa endelevu, ili kuweza kusaidia jamiii ambayo kwa kiasi kikubwa inatumika barabara bila kuwa na elimu ya kujikinga na hatari zilizopo barabarani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live