Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watendaji wapewa siku 7 kuorodhesha wakulima

74050733c96bd1d147ccba3604722d8c Watendaji wapewa siku 7 kuorodhesha wakulima

Mon, 13 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKUU wa Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga ametoa siku saba kwa watendaji wa vijiji wa Halmashauri ya Ushetu kuorodhesha wakulima na ekari za ardhi wanazolima ili waweze kunufaika na mpango wa pembejeo bure.

Kiswaga aliyasema hayo jana kwenye uzinduzi wa msimu wa kilimo kwa mwaka 2021/22 katika Halmashauri ya Ushetu, alipokuwa akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali ngazi ya vijiji na kata, akasema kulima ni lazima sio hiyari.

“Nimeshangazwa hata na bajeti ya halmashauri ya Ushetu shilingi bilioni 1.8, hiyo fedha ni kidogo tuwekeze kwenye kilimo kwani chama kikuu cha ushirika wilayani Kahama (KACU) kinaweza kununua hadi kilo milioni 25, na serikali inagawa pembejeo bure isipokuwa zao la choroko watanunua kwa kilo moja shilingi 400," alisema.

Alisema Ushetu ni asilimia 56 ya eneo lote la wilaya ya Kahama na kuna kata 20 na vijiji 112, hivyo watendaji waorodheshe wakulima wote ili kurahisisha ugawaji wa pembejeo.

Kwa mujibu wa Kiswaga, idadi ya watu katika halmashauri ni 400,000 lakini ni tani nane tu za zao la pamba zililimwa msimu unaoisha.

“Takwimu zinaonesha wakulima ni 200 tu. Tunahitaji idadi iongezeke. Sitawavumilia wavivu,”alisistiza.

Makamu Mwenyekiti wa KACU, Geoffrey Mbuto alisema kwa msimu wa pamba wa mwaka huu imetenga asilimia 30 ya mbegu bora za pamba japo Bodi ya Pamba imesema kiasi kiongezwe.

Katibu wa CCM wilaya ya Kahama, Emanuel Mbamange aliwataka wananchi kutambua mchango wa maofisa kilimo na kuwatumia ipasavyo ili kuwa na uzalishaji wenye tija, hivyo kuinua uchumi wao na wa taifa.

Mtendaji wa Kijiji cha Igunda Kata ya Igunda, Bertha Masika, alisema kazi ya kuorodhesha itakuwa rahisi kwani wakulima watajitosheleza kwa wingi baada ya kusikia pembejeo zinatolewa bure.

Chanzo: www.habarileo.co.tz