Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watendaji wanusurika kunyakuliwa na OCD

Dc Njiombe.jpeg Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Kissa Kasongwa.

Wed, 11 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe walioshindwa kutekeleza vizuri zoezi la kuweka vibao kwenye mitaa na nyumba katika zoezi la anwani za makazi linaloendelea nchini wameponea chupu chupu kuchukuliwa na mkuu wa polisi wilaya (OCD) mbele ya kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo ili waweze kushughulikiwa kutokana na kushindwa kutekeleza zoezi hilo.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ametoa siku mbili kwa watendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanakwenda kupandisha kiwango cha zoezi la anwani za makazi kutokana na hadi sasa kufikia 14% pekee ya uwekaji wa vibao vya barabara na mitaa na kuwa nje ya lengo lililokusudiwa.

“Bado tuko nyuma,nilikuwa niwachukulie hatua kwa mtendaji ambaye hakijabandikwa kibao hata kimoja kwa kuwa nimefanya hivyo Njombe mjini,sasa hapa nawapa siku mbili nione mabadiriko,lengo la kuweka nguzo ni 1980 lakini nguzo zilizosimikwa ni 284 sawa na 14.34% tuko chini”alisema Kissa Kasongwa

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli amewaagiza madiwani wote kwenda kuitisha kikao cha dharura cha baraza la maendeleo ya kata (kamaka) ili kujadili utekelezaji wa zoezi hilo la anwani za makazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live