Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watekeleza agizo la kutengeneza madawati

0a4fb1361d3841209bde8b6e7b938afc.jpeg Watekeleza agizo la kutengeneza madawati

Sun, 18 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KATA ya Dung’unyi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida imetekeleza agizo la serikali kwa kutengeneza madawati na kuhakikisha wanafunzi wote walioanza kidato cha kwanza mwaka huu wanakwenda shuleni na wanakaa kwenye viti.

Madawati hayo yamepatikana kutokana na nguvu za wananchi.

Akizungumza juzi wakati akikabidhi madawati hayo Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Yahaya Njiku aliwapongeza wananchi kwa kutengeneza madawati hayo kwa nguvu zao.

Alisema hatua hiyo waliifikia kufuatia ongezeko kubwa la ufaulu wa watoto na kuhakikisha wote wanakwenda shuleni na kuwa na viti vya kukalia.

“Nakabidhi madawati mapya 18 hapa Shule ya Sekondari Munkinya katika kata hii ya Dung’unyi ikiwa ni awamu ya pili baada ya awamu ya kwanza kukabidhi madawati 20 na idadi ya madawati yote kufikia 38 huku madawati zaidi ya 70 yakikarabatiwa… kwa nchi nzima halmashauri yetu imekuwa ya 78 kati halmashauri 195 zilizopo kwa kutengeneza madawati tunakila sababu ya kujivunia na naamini kabisa ipo siku na sisi tutashika nafasi ya kwanza,” alisema.

Mkuu wa shule hiyo ya Sekondari ya Munkinya, Faraja Mlelwa aliwashukuru wadau wa maendeleo waliochangia upatikanaji wa madawati hayo na kuwa watayatunza.

Lengo la halmashauri hiyo ni kuhakikisha madawati yote 3,900 yanapatikana na kuwa watoto hao wote wanafika chuo kikuu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz