Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu wanusurika kifo wakishambuliwa na tembo

Wajeruhiwapicc Data Watatu wanusurika kifo wakishambuliwa na tembo

Sat, 1 Oct 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mtu mmoja amelazwa katika ya Hospitali ya Wilaya ya Kiteto na wengine wawili kunusurika kifo baada ya kushambuliwa na tembo eneo la Pori kwa Pori Kijiji cha Olpopong Kata ya Njoro mkoani Manyara leo Oktoba Mosi, 2022.

Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, George Katabazi akisema wananchi wachukue tahadhari dhidi ya wanyama hao wanaotoroka maeneo ya hifadhi.

Muunguzi wa hospitali ya Wilaya ya Kiteto ambaye hakutaka jina lake litajwe, amekiri kupokea majeruhi watatu na kwamba wanaendelea vizuri na matibabu.

Akizungumza hospitali hapo, mmoja wa majeruhi hao,

Akizungumza akiwa hospitalini hapo, mmoja wa majeruhi hao, Mathayo Jeseph Gwabu amesema wamekuwa wakitumia maji ya bwawa hilo kwa matumizi ya nyumbani na kunweshea mifugo.

"Tuliamka alfajiri ya saa 10 kwenda kuchota maji bwawa la Pori kwa Pori, ambalo huwa tunalitumia kwa kushirikiana na mifugo na hata wanyamapori wakati mwingine hulitumia.

“Tuliwakuta tembo wakinywa maji, nao walipotuona wakaanza kutukimbiza na kunijeruhi mimi niliyekuwa mbele na baiskeli. Tembo alinifukuza nyuma mpaka nikaanguka kisha kutumia pembe yake kunichoma kifuani hadi ikatokea mgongoni," amesema majeruhi huyo.

Kwa upande wake Fredson Bira, amesema kwa kipindi hiki tembo wamekuwa tishio katika maeneo ya Kiteto.

“Pamoja kwamba taarifa zilifikiwa mamlaka husika kipindi chote huwa wanaswagwa kurejeshwa porini, huku viongozi wao wakitutaka tuchukue tahadhari na kuwakwepa wanyama hao wanapokuja kwenye maeneo yetu,” amesema.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz