Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu wakamatwa na meno ya tembo Tanga

Images (1).jpeg Meno ya tembo

Wed, 22 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watatu wamekamatwa na meno matano ya tembo yanayodhaniwa kuwa na kilogramu 24 katika kijiji cha Manolo kata ya Shume wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga.

Akithibitisha kukamatwa kwa watu hao mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na mkuu wa wilaya hiyo, Kalisti Lazaro amesema watu hao wamekamatwa leo June 20,2022 saa saba mchana kjiji cha Manolo wilayani humo wakiwa wamepakia meno hayo katika pikipiki.

Kalisti amesema kuwa watu hao wamekamatwa na Inspector Pesa wa Ofisi ya RCO Kilimanjaro aliyekuwa kwenye operation Maalum na Askari wenzake pamoja na askari wa Tanapa.

Aliwataja waliokamatwa ni Hassan Shauri (73) Mkazi waManolo ,Eliud Gadi (32) Mkazi wa Manolo Godson Elikunda (27) dereva wa pikiki na Mkazi wa manolo.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama amesema kuwa watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa nakwamba wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema serikali ya wilaya ya Lushoto Iko macho nakwamba itawakamata wale wote eatakaoendelea kujihusisha na biashara hiyo ya nyara za Serikali.

Hata hivyo alitoa wito Kwa wananchi kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na biashara za namna hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live