Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu wahukumia kunyongwa Tanga

Hukumu Pc Data Watatu wahukumia kunyongwa Tanga

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limesema kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita Watuhumiwa wa Watatu wa Mauaji ambao ni Rashid Mwalimu (Chid Kiwanga), Siwajui Kigaa (Sahonelo) (27) na Zuberi Hassan (34) wote wakiwa wakazi wa Kijiji cha Kwandugwa, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wamehukumiwa kunyongwa hadi Kufa kwa kosa la Mauaji ya Mtoto wa Kike mwenye umri wa Miaka Tisa.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Almachius Mchunguzi wakati akitoa Taarifa kwa Vyombo vya habari kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Oktoba 22, hadi November 27 mwaka 2023

Kamanda Mchunguzi amesema Jumla ya Watuhumiwa 41 wamefikishwa mahakamani, kesi 11 zinaendelea mahakamani na kesi 27 zimetolewa hukumu mbalimbali ambapo Watuhumiwa watatu ambao ni Justis Kunael (40), Saidi Adam (32), na Maliki Amiri (38) wote wakazi wa Handeni wamehukumiwa kifungo cha Maisha kwa kosa la kubaka

Vile Vile Kamanda Mchunguzi amesema November 18, 2023 wamefanikiwa kumkamata Hamis Kombo (46) mkazi wa Kwediboma Wilaya ya Kilindi akiwa ma Wenzake nane wote waganga wa kienyeji wanaojihusisha na Ramli Chonganishi wakiwa katika katika kijiji cha Kivindani, kata ya Tongoni tarafa ya Pongwe wilaya ya Tanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live