Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu wahofiwa kufa maji Ziwa Victoria

Watatu Pic Data Maji Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibushubwamu

Mon, 28 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watatu wanahofiwa kufariki dunia huku mmoja akinusurika baada ya mtumbwi waliokuwa wakitumiwa kuvua samaki kupigwa na dhoruba na kuzama.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Februari 28, 2022  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibushubwamu amesema kuwa tukio hilo lilitokea Ijumaa iliyopita ndani ya ziwa Victoria katika kisiwa cha Rukuba wilayani Musoma.

Kamanda Tibushubwamu amesema kuwa siku hiyo wavuvi wanne waliingia ziwani usiku kuvua dagaa lakini wakiwa wanaendelea na shughuli zao ghafla yaliibuka mawimbi makubwa ziwani na kupelekea mtumbwi wao kupigwa na dhoruba na kupasuka kisha kuzama majini.

Amewataja watu wanaohofiwa kufariki dunia kuwa ni pamoja na Kaida Mafuru (37), Frank Magwinya 35 na mtu mwingine anayetambulika kwa jina moja la Jeti (30).

Amesema kuwa aliyenusurika ni Peter Willim (35) baada ya kufanikiwa kushika ubao uliopasuka kutoka mwenye mtumbwi hivyo kuelea ziwani hadi asubuhi alipookolewa na amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Mara akiendelea na matibabu.

"Hawa watu watatu hatuna uhakika kama wamefariki au la kwasababu hadi sasa bado hawajapatikana tangu tukio lilivyotokea lakini oparesheni inaendelea ziwani kuwatafutwa aidha wawe wamekufa au wako hai na hivi tunavyoongea boti kadhaa zipo eneo la tukio zikiendelea kuwatafuta" amesema Kamanda Tibushubwamu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live