Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu wafariki kwa kufukiwa na kifusi Sikonge

Kifusi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Watu watatu wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi katika Kijiji cha Misheni wilayani Sikonge.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema watu hao walifariki jana Jumanne Novemba 16, 2021 wakati wakati wakichimba mchanga.

"Chanzo ni kuporomoka kwa kifusi au udongo na kuwaangukia wakati wakiwa chini wanachimba udongo" amesema.

Kamanda Abwao ameeleza kuwa shimo lililosababisha vifo ni mabaki ya mojawapo wa mashimo yaliyochimbwa katika ujenzi barabara.

Amewataja waliofariki kuwa ni Bakari Shaban (21), Sadick Ramadhan (9) na Rashid Hamis (9) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu Katika Shule ya Msingi Majengo.

Kamanda Abwao amewataka wananchi kuwa waangalifu wanapochimba udongo katika mashimo.

Chanzo: mwananchidigital