Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu wafariki dunia katika ajali Moshi

15260 Pic+ajali TanzaniaWeb

Mon, 3 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Watu watatu wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa, mkoani Kilimanjaro baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso katika eneo la Hedaru, wilaya ya Same mkoani humo.

Akizungumza na Mwananchi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Hamis Issah, amesema ajali hiyo imetokea jana usiku majira ya saa 5:55 usiku, Septemba 2, 2018 katika kijiji cha Hedaru bababara kuu ya Tanga-Arusha.

Kamanda Issah amesema ajali hiyo imehusisha magari mawili moja aina ya  Toyota Canter iliyokuwa ikitokea Lushoto kwenda Arusha na Scania iliyokuwa ikitokea Makanya kwenda Tanga.

Amesema waliofariki ni madereva wote wawili na utingo mmoja na majeruhi ni utingo mmoja.

Chanzo: mwananchi.co.tz