Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu mbaroni kwa kufanya biashara ya binadamu Mbeya

MBARONI.jpeg Watu watatu mbaroni

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: Mwananchi

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuwasafirisha watoto wenye umri wa miaka 10 na kuwapeleka kutumikishwa kazi majumbani, kilimo na ufugaji katika maeneo mbalimbali.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Urlich Matei amesema leo Septemba 7, 2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa jana wakati wakiwa kwenye harakati za kuwasafirisha kuwapeleka kwa wakulima na wafugaji wilayani mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kutumikishwa kazi, ambapo kwa kila mtoto mmoja walikuwa wakilipwa kiasi cha Sh20,000 mpaka Sh25,000.

"Imebainika kuwa watuhumiwa hao, kwa makubaliano yao kila mtoto mmoja aliyekuwa akiafirishwa wanapatiwa ujira wa Sh20,000 mpaka 25,000 bila kutambua kuwa kufanya biashara ya binadamu na kuwatumikisha watoto ni kinyume cha sheria," amesema.

Amesema kuwa polisi bado wanaendelea na mahojiano na watuhumiwa na watafikishwa mahakamani wakati wowote uchunguzi utakapokamilika.

Mkurugenzi wa asasi isiyokuwa na kiserikali ya Sauti ya Mama Afrika (Samofa), Thabitha Bughali ameomba Serikali kuchukua hatua kali kwani kitendo hicho ninawanyima haki watoto kupata elimu na kujikuta wakinyanyaliwa kwa jamii.

Chanzo: Mwananchi