Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania kumkumbuka Magufuli kuboresha huduma za kijamii

Maji Mag Watanzania kumkumbuka Magufuli kuboresha huduma za kijamii

Thu, 25 Mar 2021 Chanzo: ippmedia.com

Aidha, mbali na huduma hizo kwenye vijiji hivyo, pia Rais hatasahaulika na taifa la Tanzania kutokana na maono yake ya kuanzisha miradi mikubwa ili kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa kwa ajili ya maendeleo yake ikiwemo kutumia rasilimali zilizopo nchini.

Katibu Msengi, amesema hayo alipokuwa akizungumza na Nipashe kuhusu kifo cha aliyekuwa Rais hayati Dk. John Magufuli aliyefariki machi 17, mwaka huu jijini Dar-es-salaam.

Amesema kuwa, kuna baadhi ya vijiji vingi hapa nchini ambavyo toka nchi ipate uhuru havijawahi kuona huduma kama vile ya umeme, maji salama, barabara na vituo vya afya lakini hayati Dk. Magufuli leo amevifanikisha kupata maendeleo hayo.

Amese,a pamoja na kuwakomboa wananchi hao wa vijijini kwenye huduma hizo hayati Magufuli, pia alikuwa na maono makubwa ya kuanzisha miradi mikubwa ambayo itakayowaondolea watanzania tunaamini itatuondolea umasikini na kuwawezesha kukua kiuchumi.

“Pia tutaweza kumkumbuka kwa hili la matumizi ya fedha nalo limekuwa na nidhamu ya hali ya juu, hii ni pamoja suala zima la kila mtanzania kumtaka kufanya kazi kwa bidii tofauti na huko nyuma ambapo watu walikuwa wakishinda vijiweni na maisha ya ubabaishaji,” amesema.

Chanzo: ippmedia.com