Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watano wapoteza maisha kwa ajali ya gari

11858 PIC+AJALI TanzaniaWeb

Tue, 14 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Rorya/Mwanza. Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Busurwa mwambao wa Ziwa Victoria wilayani Rorya kwenda mjini Tarime kupinduka.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tarime na Rorya, Henry Mwaibambe amesema ajali hiyo ilitokea katika kitongoji cha Bukwe eneo la Mika alfajiri ya leo Agosti 14, 2018.

“Uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha ajali ni mwendo kasi uliosababishwa na dereva aliyekuwa akiwakimbia askari wa doria. Alikataa kutii amri ya kusimama kutokana na kubeba samaki wanaosadikiwa kupatikana kutokana na uvuvi haramu,” amesema Kamanda Mwaibambe.

Akizungumza na Mwananchi akiwa eneo la tukio, amesema majina ya waliokufa bado hayajatambuliwa na miili imehifadhiwa katika Kituo cha Afya cha Utegi wilayani Rorya ambako pia majeruhi wamepelekwa kwa matibabu.

Kamanda Mwaibambe amemtaja dereva wa gari hilo kuwa ni Athumani Masiaga ambaye ni miongoni mwa waliofariki dunia.

Mmoja wa watu walioshuhudia ajali aliyezungumza na Mwananchi, Jacob Adongo amesema abiria waliokuwamo kwenye gari ni wafanyabiashara wa samaki kutoka wilaya za Tarime na Rorya mkoani Mara.

Chanzo: mwananchi.co.tz