Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watano wafariki kwa ajali ya boti Rufiji

Watano Wafariki Kwa Ajali Ya Boti Rufiji Watano wafariki kwa ajali ya boti Rufiji

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wavuvi watano wamefariki dunia na wengine wawili hawajulikani walipo baada ya boti waliyokuwa wakitumia katika shughuli za uvuvi kugonga kingo za mto Rufiji kisha kupinduka wilayani mafia mkoani Pwani.

Boti hiyo ambayo ilikuwa imebeba wavuvi 15 ilikuwa inatoka Mafia kwenda Kibiti.

Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Zephania Sumaye akizungumza kwa njia ya simu na Mwananchi Digital leo Alhamisi Novemba mosi, 2023 amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema boti hiyo ilikuwa na watu 15 ambapo 12 walikuwa wanawake na watatu wanaume.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live