Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watano wa familia moja wafariki ajalini

Ulrich Matembe Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Mbeya SACP Ulrich Matei

Tue, 21 Sep 2021 Chanzo: Mwananchi

Watu watano wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa katika ajali ambayo imetokea eneo la Imezu wilayani Mbeya baada ya lori lenye namba za usajili T 616 DEX kuyagonga magari mengine mawili na kisha kupinduka.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Mbeya SACP Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu watano wa familia moja waliokuwa wakitokea msibani wilayani Mbozi mkoani Songwe kuelekea Morogoro.

Ajali hiyo imetokea leo Septemba 21, 2021 , Ulrich Matei amesema watatu wamefariki papo hapo na wawili wamefia Hospitali.

Chanzo: Mwananchi