Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakiwa kutoruhusu watu kutoka nchi jirani kuingia njia ya panya 

Huuu Watakiwa kutoruhusu watu kutoka nchi jirani kuingia njia ya panya 

Sat, 3 Jul 2021 Chanzo: ippmedia.com

..... kwa kufuata taratibu zote wanazoelezwa na wataalamu wa afya na kutoruhusu watu kutoka nchi jirani kuingia kwa kutumia njia za panya. 

Akizungumza katika ibada ya kuwasimika wachungaji watatu na viongozi wa vijana iliyofanyika katika Kanisa la Calvary Assemblies of God (CAG) lililopo Chonyonyo wilayani Karagwe, Askofu wa CAG Jimbo la Kagera, Damian Rwabutikula amesema kuwa ili kudhibiti maambukizi ya corona wananchi wote na viongozi wanapaswa kuchukua tahadhari kwa kuzingatia maelekezo ya kitaalamu.

Aidha Askofu Rwabutikula amewataka wachungaji wa kanisa hilo kutoa elimu sahihi kwa waumini wao ya namna ya kujikinga na kuhakikisha wanakaa bila kubanana, kunawa mikono kwa sabuni na kuvaa barakoa wanapokuwa katika mikusanyiko ikiwamo ibada.

Amesema wachungaji hao wanatakiwa kuzingatia masharti na maelekezo ya wataalamu wa afya katika utendaji wao wa kutoa huduma za kichungaji, kutokana na mkoa huo kuwa mpakani, hivyo kuna hatari ya kupata waumini wageni kutoka nchi jirani.

Pia amewataka wananchi kuacha woga yanapotokea majanga katika jamii, maana woga unasababisha kufanya maamuzi yasiyo sahihi, na badala yake wanatakiwa kufuata maelekezo wanayopatiwa na watawala wakati huo wakiendelea kumuomba Mungu.

Naye Katibu wa kanisa hilo Mkoa wa Kagera, Mchungaji Agnes Charles amewataka wachungaji kuwa na utamaduni wa kujiendeleza kielimu kwa kushiriki mafunzo mbalimbali ya uongozi, ili kujikumbusha miiko na maadili katika kazi yao.

Katibu msaidizi wa CAG kanda ya Mashariki, Askofu Amos Peter kutoka jijini Dar es Salaam ametumia fursa hiyo kuwaonya wachungaji kuacha tabia ya kushabikia jambo lolote linaloipinga serikali, akidai kufanya hivyo kutawapunguzia uaminifu kwa serikali na jamii kwa ujumla.

Chanzo: ippmedia.com