Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakiwa kutambua majukumu yao ya kazi

F7a8798fede0a1859eb3d17ed1d85dcc Watakiwa kutambua majukumu yao ya kazi

Thu, 26 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amewataka Wanataluma wa ustawi wa jamii kuhakikisha wanafanya kazi kwa kutambua majukumu yao. Rai hiyo imetolewa wakati Mongela alipokuwa akizindua mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha wanataluma ya ustawi wa jamii(TASWO).

Alisema maofisa wa ustawi wa jamii wanatakiwa kushiriki pia katika kusaidia watu kwenye majanga mbali mbali yanapotokea kama moto, majanga ya njaa, mafuriko na ajali.

Aliwapongeza maofisa ustawi wa jamii wa mkoa wa Mwanza kwa kujitoa na kuwasaidia wakazi wa kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe wakati wa ajali ya Mv Nyerere.

Kamishina wa ustawi wa jamii kutoka Wizara ya Afya jinsia na watoto, Naftali Ng’ondi aliwataka watalamu wa ustawi wa jamii kufanya kazi kwa pamoja katika kusaidia watu mbali mbali wenye shida.

Alisema maofisa wote wa ustawi wa jamii wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi. Ameitaka Taswo kuhakikisha inawajengea uwezo watumishi wake kwa kuandaa semina na mafunzo mbali mbali pamoja na kushirikisha wadau.

Aliwaagiza maofisa ustawi kuvifungia vituo vya kulelea watu visivyokuwa na sifa ya kulea watoto.

Makamu mwenyekiti wa Taswo,Awadh Mohamed alisema kupitia mkutano huo watapata muda wa kujadili mpango kazi kwajili ya mwakani pamoja na kuendeleza mafanikio mbali mbali ya chama chao.

Mratibu mpango wa malezi mbadala katika jamii kutoka asasi isiyokuwa ya kiserikali SOS children village Tanzania,Husna Selungwi alisema wataendelea kushirikiana na Taswo katika kuboresha huduma za malezi kwa watoto waliokosa malezi.

Chanzo: habarileo.co.tz