Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakiwa kujiunga kupata mikopo

8dcac9d5bbb82465feb41897be5f176e Watakiwa kujiunga kupata mikopo

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WANAWAKE wanaojishughulisha na biashara mkoani Tabora wametakiwa kujiunga katika vikundi ili waweze kunufaika na fursa za mikopo isiyo na riba inayotolewa na serikali kupitia halmashauri za wilaya na Shirika la Viwanda Vidogo nchini (SIDO).

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wafanyabiashara Wanawake Mkoani hapa, Amina Madereka katika Mkutano wa Chama hicho wa kufunga mwaka uliofanyika jana katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Alisema kuwa wanawake wengi wanafanya vizuri katika biashara lakini changamoto kubwa ni mitaji ya kuboresha bidhaa zao, hivyo akawataka kujiunga katika vikundi ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na halmashauri zote hapa nchini ili kuboresha bidhaa zao.

“Naomba kila mwanawake anayejishughulisha na biashara ajiunge katika kikundi ili aweze kupata mkopo usio na riba utakaomsaidia kuboresha bidhaa zake ili kujikwamua kiuchumi,” alisema.

Mratibu wa Wajasiriamali mkoani hapa Ashura Mwazembe alibainisha kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanywa na baadhi ya wanaume kwa wake zao vimekuwa vikichangia baadhi ya wanawake kushindwa kufikia malengo yao kibiashara.

Aliiomba mamlaka husika za serikali kuwachukulia hatua stahiki wale wote watakaobainika kuwafanyia vitendo vya ukatili au kuwanyanyapaa wanawake kwa kuwazuia kujiunga na vikundi vya wenzao ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Chanzo: habarileo.co.tz