Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakiwa kubuni mikakati ya kukabili ukatili

F5ebb03e848abaf167f88018f7862e96 Watakiwa kubuni mikakati ya kukabili ukatili

Sat, 5 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Mke wa Waziri Mkuu wa zamani, mama Tunu Pinda amewataka wanawake wa mtandao wa wanawake laki moja kuhakikisha wanakuja na mbinu mbali mbali za kuhakikisha wanatokomeza na kumaliza tatizo la ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

Rai hiyo aliitoa wakati wa uzinduzi wa mtandao huo wa wanawake katika mkoa wa Mwanza, Pinda alisema mtandao huo unatakiwa kuja na mbinu ya kutoa elimu endelevu katika kubadilisha mitazamo ya watu ili waweze kuacha tabia ya ukatili.

Alisema anawataka wanawake kuhakikisha wanatumia fursa mbali mbali za Serikali ikiwemo kuchukua mikopo katika Halmashauri na kuweza kujiajiri.

Pinda ameitaka jamii kuachana na mila potofu zinazoathiri mila za wanawake. Ameupongeza mtandao wa wanawake laki moja kwa kufungua ofisi zao katika mikoa 17 hapa nchini.

Katibu mkuu wa mtandao wa wanawake laki moja,Josephine Kiongoda alisema lengo kuu la mtandao wao ni kuunganisha wanawake nchi nzima pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia.

Alisema kwa sasa nchi nzima wanao wanachama 3084 na lengo lao ni kufikisha wanachama 100,000. Alisema mtandao wao una lengo la kuhakikisha inawafikia wanawake mikoa yote.

Mwenyekiti wa mtandao wanawake laki moja jijini Mwanza,Winfrida Gyunda alisema wataendelea kupambana na kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

Alisema mtandao wao kwa mkoa wa Mwanza kuna wanachama 400.

Mwenyekiti wa mtandao wanawake laki moja jijini Dar-es-salaam,Wakili Suzana Senso alisema jiji la Dar linakabiliwa na unyanyasaji uliojificha na kuna changamoto kubwa ya malezi.

Chanzo: habarileo.co.tz