Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watahiniwa Shule ya Bwisya wakumbushia ya Mv Nyerere

27093 Pic+wanafunzi TanzaniaWeb

Wed, 14 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Leo ni Novemba 14, 2018 sawa na siku 55 tangu kutokea kwa ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyowaangamiza watu 230 huku 41 wakinusurika huku Shule ya Sekondari Bwisya ikipoteza jumla ya wanafunzi 11.

Ajali hiyo iliwaua watu 230, kati ya hao, 88 walitoka kaya 73 kati ya 600 kwenye kata ya Bwisya, wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu diwani wa kata ya Bwisya, Disma Busanya amesema kati ya watu 88 walioangamia ziwani, wengi walikuwa wanawake.

“Imekuwa ni bahati mbaya na tunaishukuru Serikali iliweza kwenda mbele zaidi kwa kuwapa mkono wa pole waathirika wote wa mkasa huu ingawa nafasi ya binadamu haina thamani ya fedha,” amesema diwani.

Pamoja na kusababisha vifo kwa wananchi wa kawaida, ajali hiyo pia ilisababisha maafa makubwa kwa Shule ya Sekondari ya Bwisya iliyopoteza wanafunzi ambao kati yao wawili walitakiwa kufanya mtihani wa kidato cha pili unaoendelea kote nchini.

Kaimu mwalimu mkuu wa Shule ya Bwisya, Emmanuel Minja, amesema shule hiyo iliwapoteza wanafunzi 11 kwa ujumla. Amewataja wanafuzi hao kuwa ni Albinus Busanya na Anita Nyangoro, wote wa kidato cha pili.

“Awali tulikuwa na watahiniwa 282 lakini baada ya ajali ya MV Nyerere, tumebaki na watahiniwa 280 na ndio hao wamefanikiwa kufanya mtihani wa kidato cha pili,” amesema Minja.



Chanzo: mwananchi.co.tz