Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watafiti watakiwa kutatua changamoto za jamii

E20aec4860b051be388a2c79c55c4f47 Watafiti watakiwa kutatua changamoto za jamii

Sun, 22 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amewataka watafiti kufanya kazi zao vyema kwa lengo la kutatua changamoto zinazojitokeza katika jamii .

Alisema hayo wakati akizungumza katika kongamano la kitaaluma lilioandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE),

Alisema wakati umefika kwa watafiti watanzania kujikita katika kutatua matatizo ya watanzania badala ya kutegemea watafiti wa nje ambao wanafanya kwa makusudio yao binafsi.

"Wakati mwingine najua huwa tunapata wasimamizi kutoka nje ya nchi ambaye kwenye kuchagua hiyo research topic (mada ya utafiti) yako anaweza kuwa na mwonekano wa upendeleo wa upande wake,"alisema.

Aidha katika hotuba yake aliwapongeza CBE kwa kufanya utafiti katika eneo la wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama machinga ambao unalenga kutatua changamoto walizonazo.

Naye mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Ali Gugu alisema machapisho yanayotolewa na chuo hicho yanalenga katika kuisaidia jamii na Taifa kwa ujumla.

Awali, Mkuu wa Chuo Cha CBE, Profesa Emanuel Mjema alisema chuo kimeendelea kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa ushauri katika sekta ya viwanda na biashara.

Alisema moja ya changamoto ya juu iliyoibuliwa na tafiti hizo ni ya kurasimisha shughuli za wafanyabiashara ndogo ndogo ili kukuza mitaji yao pamoja na kuchangia pato la Taifa kupitia ulipaji wa kodi.

"Machinga tunafikiri ni biashara ndogo lakini kumbe ni biashara kubwa na inahusisha watu wengi sana kwa hiyo inatoa ajira nyingi sana kwa hiyo tukiirasimisha inaweza kuchangia kodi katika nchi yetu,"alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz