Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watafiti SUA watahadharisha wafugaji kongwa, Singida

0e49c9db3555ef9848c3af613482ea97 Watafiti SUA watahadharisha wafugaji kongwa, Singida

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwa kushirikiana na Serikali wamesema kuna haja ya kuchukua hatua za haraka za kudhibiti kusambaa kwa mmea wa Gugu Kongwa ambao umeonesha kuathiri kwa kiasi kikubwa maeneo ya malisho yaliyopo wilayani Kongwa na Mkoani Singida.

Hayo yamebainishwa na Wataalamu hao walipokutana na wadau wengine wa Sekta ya mifugo jijini Dodoma kuwasilisha matokeo ya awali ya utafiti waliofanya kujua tabia za ukuaji na usambaaji wa mmea huo ili kutafuta njia fungamanishi za kupunguza au kutokomeza kabisa mmea huo ujulikanao Gugu Kongwa.

Akiongea katika Mkutano huo, Mtafiti Kiongozi kutoka SUA, Dk Selemani Ismail amesema utafiti wa Gugu Kongwa ulilenga kujua tabia ya ukuaji wake na kwa kiasi gani mmea huo unaoathiri malisho ya Mifugo umesambaa.

Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Utafiti, Mafunzo na Huduma za Ugani kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Kejeri Gillah amesema kuwa Wizara kwa kushirikiana na wadau wengine inajipanga kuhakikisha matokeo hayo ya utafiti yanakwenda kufanyiwa kazi.

Naye, Meneja wa Mfuko wa Kuendeleza Sayansi na Teknolojia kutoka COSTECH, Ntufye Mwakigonja amesema anaimani kuwa utafiti huo utatatua changamoto hiyo inayokabili malisho nchini huku akiongeza kuwa wao kama COSTECH wataendelea kushirikiana na watafiti hao ili kuhakikisha matokeo hayo yanafanyiwa kazi kwa manufaa ya Sekta ya mifugo nchini.

Aidha, Wadau wa Sekta ya Mifugo waliohudhuria mkutano huo wamesema kuwa pamoja na kuwepo changamoto zinazosababishwa na mmea huo katika malisho ya mifugo, watafiti hao waendelee kufanya utafiti kuangalia mtizamo chanya ambao unaweza kusaidia jamii kutumia faida zinazoweza kupatikana zitokanazo na Gugu Kongwa

Chanzo: www.habarileo.co.tz