Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasiozidi 10 kuuzika mwili wa DC Mtwara

EVODI Wasiozidi 10 kuuzika mwili wa DC Mtwara

Tue, 28 Apr 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UONGOZI wa Mkoa wa Mtwara, umesema mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evodi Mmanda, yatafanyika Mtwara chini ya usimamizi wa serikali na kuhudhuriwa na watu wasiozidi 10.

Umesema hatua hiyo imechukuliwa kwa lengo la kuzingatia na kusimamia taratibu za Wizara ya Afya kuzuia mikusanyiko katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, aliyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari na kueleza taratibu za mazishi ambayo hata hivyo hakutaja tarehe ya kufanyika kwake.

Alisema kutokana na taratibu za tahadhari ya corona zilizoelekezwa na Wizara ya Afya, serikali inalazimika kuzika mwili huo na mazishi yake yatahudhuriwa na watu wasiozidi 10 ili kuwa na hadhari ya maambukizo ya ugonjwa wa corona.

Alisema familia ya marehemu imetoa ushirikiano mkubwa na taratibu za kuuhifadhi mwili zinaendelea na kuwasisitiza wananchi wa Mkoa wa Mtwara kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.

Alisema Mmanda alianza kujisikia vibaya Ijumaa akiwa ofisini na hivyo kulazimika kwenda kupata matibabu katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa (Ligula) na hali ilivyozidi kuwa mbaya, alilazimika kulazwa mpaka juzi majira ya saa tano usiku alipoaga dunia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live