Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasimamishwa kazi kisa wizi wa TV za hospitali

Mtakataka.jpeg Wasimamishwa kazi kisa wizi wa TV za hospitali

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ameagiza kuwasimamisha kazi baadhi ya watumishi katika hopitali ya rufaa ya mkoa wa Njombe akiwemo katibu wa afya,watu wa idara ya manunuzi pamoja na idara ya tehema ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za wizi wa Runinga 15 zenye thamani ya sh. Mil. 11 pamoja na kompyuta tatu katika hospitali hiyo.

Mkuu huyo wa Mkoa amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa wizi huo tangu mwezi Julai mwaka huu pasipo kuripotiwa kwenye chombo chochote cha ulinzi na usalama huku idara ya Tehama ikishindwa kutambua chochote kutokana na Kamera kutofanya kazi.

Aidha imedaiwa kuwa wizi huo umlifanyika kwa kufungua kontena lililokuwa na vifaa hivyo katika siku ambazo sio za kazi na baada ya kubainika tatizo hilo mkuu wa Idara ya manunuzi wa Hospitali hiyo pamoja na watunza funguo wenzake wakamua kukubaliana kuzilipa kwa kwenda kumuomba mfanyabiashara wa vifaa vya umeme mjini Njombe ili awape Runinga 15 nyingine ambazo watazilipa katika siku za usoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live