Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasichana 8,000 wapata ujauzito Mtwara

Mimba Mashuleniiii Wasichana 8,000 wapata ujauzito Mtwara

Thu, 9 Mar 2023 Chanzo: Habarileo

Imeelezwa kuwa wasichana 8,000 wenye umri kuanzia miaka 10 hadi 19 wamepata ujauzito kuanzia Januari mpaka Disemba 2022 katika Mkoa wa Mtwara. Tatizo hilo limetajwa kuwa ni kubwa mkoani humo.

Akizungumza leo Machi 8, 2023 wilayani Tandahimba katika Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amesema takwimu hizo ni kwa mujibu wa takwimu za mfumo wa taarifa na upashaji habari za afya za mkoa.

‘’Bado mtoto wa kike anapitia vikwazo vinavyoweza kukwamisha kupata elimu na pengine hata kukatisha masomo yake kwani miongoni mwa vikwazo hivyo ni pamoja na mimba za utotoni hili ni tatizo kubwa katika mkoa wetu’”.Amesema Abbas.

Amesema kwa takwimu hizo inaonesha kuwa bado kuna tatizo kubwa la mimba hizo za utotoni katika kila halmashauri mkoani humo ambapo asilimia zaidi ya 19.4 ya wajawazito wote wanaopata huduma katika vituo vya afya mkaoni humo ni watoto waliochini ya umri wa miaka 19.

‘’Tukumbuke kuwa mimba za utotoni huathiri afya, elimu na haki za mtoto wa kike mtoto wa kike aliyekosa elimu kuna changamoto katika kupata ajira na kushindwa kujenga maisha bora katika Familia yake’’,

Mkuu huyo wa mkoa ametoa wito kwa Jamii, taasisi zisizo za Kiserikali pamoja na Wadau wote kwa ujumla mkoani humo kwa pamoja kushirikiana na Serikali katika kupambana na ndoa, mimba hizo za utotoni ili kuweza kufikia malengo ya kumkomba mtoto wa kike na kumuweka kwenye mazingira yaliyokuwa salama yakumwezesha kufikia ndoto zake badala ya kukatishwa na mimba za utotoni.

Mkuu wa Dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara Bahati Sembela amesema madawati hayo yapo kwa ajili ya kumpa muhanga wa ukatili usiri na ufalagha wa kuweza kutoa malalamiko yake hivyo ameikumbusha Jamii kwa ujumla kuwa na jitihada ya kufichua vitendo na matukio ya ukatili yanayojitokeza kwenye Jamii yao na kufanya hivyo itapelekea kupunguza vitendo hivyo vya ukatili vilivyoshamiri katika maeneo yao.

‘’Vitendo hivi vya ukatili vimetokea kushamiri sana katika Mkoa wetu hivyo ndiyo vinapelekea Wananchi kutokuwa na imani na jeshi la polisi lakini nasimama kurudu kwa Wananchi kuwaomba kwamba tushirikiane kwa pamoja ili tukomeshe vitendo hivi’

Chanzo: Habarileo