Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washushwa vyeo kwa kushindwa kupeleka fedha benki

Pic Fedha Data Wastaafu Washushwa vyeo kwa kushindwa kupeleka fedha benki

Tue, 13 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watumishi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora wanakabiliwa na adhabu ya kushushwa vyeo na kukatwa mishahara kwa kushindwa kupeleka fedha benki baada ya kuzikusanya.

Meya wa manispaa ya Tabora, Ramadhan Kapela amesema wamechukua uamuzi huo baada ya kikao cha baraza maalumu lililojadili taarifa ya ukaguzi maalum wa miaka mitatu kuanzia mwaka wa fedha 2017/18 hadi 2019/20 ambapo Sh81 milioni zilizokusanywa na watendaji hazikuwasilishwa benki.

Amesema wamebaini watumishi 27 watoza ushuru walikusanya ushuru katika kipindi cha miaka mitatu lakini hawakupeleka benki Sh26 milioni ambapo baadhi yao wamelipa na wengine 11 bado hawajalipa.

Kapela amesema watumishi wengine walipewa vitabu 84 ambavyo hawakuvipeleka kukaguliwa na baada ya kukaguliwa, hasara ya Sh57 milioni ilibainika.

Ameeleza baraza maalum limeazimia watumishi 69 waliohusika na hoja hizo, wakatwe mishahara kwa asilimia 15 kwa muda wa miaka 3, watumishi 27 waliolipa fedha kupewa onyo na watumishi 11 kupewa miezi miwili kurudisha na wamewashusha vyeo na mishahara.

Ameeleza hata watumishi wa idara ya fedha nao wamechukuliwa hatua kwa kukatwa mishahara kwa asilimia 15 kwa muda wa miaka mitatu.

“Katika hili hatukuwa na mzaha kwani kwa waliokuwa watendaji wa kata,tumewashusha kuwa watendaji wa mtaa pamoja na mishahara,” amesema.

Kuhusu fedha za maendeleo, amesema wamepokea zaidi ya Sh1.3 bilioni kwa ajili ya shule za Tabora Wavulana, Tabora Wasichana na Gongoni.

Ameutaka uongozi wa shule hizo na zingine kutoa taarifa za fedha wanazopata na matumizi kwa kubandika kwenye mbao za matangazo kama alivyoagiza Waziri Mkuu wiki iliyopita katika ziara yake ya siku mbili mkoani Tabora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live