Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washindi wa fasihi wafunguka

42018 Pic+fasihi Washindi wa fasihi wafunguka

Mon, 18 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Washindi wa tuzo ya Kiswahili ya Mabati- Cornell Dotto Rangimoto na Ali Hilal wameeleza kilichowavuta kuandika kabla ya kushiriki tuzo hizo mwaka 2017.

Wakizungumza kwenye hafla ya utoaji tuzo ya Kiswahili ya mabati- Cornell ya fasihi ya Afrika zinazotolewa leo Februari 15, 2019.

Dotto ambaye alishinda kwenye kitengo cha ushairi kwa mswada wake ' Mwanangu Rudi Nyumbani' amesema kuwa alianza kuandika baada ya kufiwa na mama yake mzazi.

Amesema alipofiwa na mama yake alipata maumivu makali na kuanza kuandika namna mama yake alivyoteseka na maradhi.

Amefafanua kuwa alikwenda mbali zaidi na kuandika namna mzazi anapoumwa kutoka familia masikini ambapo huuguzwa na watoto wake pekee.

"Kuanzia hapo ndiyo nilianza kuandika baada ya kuona ninaweza" amesema Rangimoto.

Kwa upande wa Ali Hilal Ali ambaye alishinda kitengo cha riwaya kwa mswada wake wa 'Mmeza Fupa'.

Hilal amesema kuwa alianza kuandika baada ya kumuona mtu ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

Amesema baada ya kupitia kilichoandikwa akavutiwa na kuamua kuandika kabla ya kushiriki tuzo, kushinda na sasa ana kitabu.



Chanzo: mwananchi.co.tz