Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washauriwa ‘kuogesha’ mifugo ili tija ipatikane

Debeb39b3533a1fc902f07c263867d41 Washauriwa ‘kuogesha’ mifugo ili tija ipatikane

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAFUGAJI wametakiwa ‘kuogesha’ mifugo yao ili kupambana na magonjwa jambo ambalo limekua likizuia Tanzania kuuza nyama katika nchi mbalimbali kutokana na viwanda vya kuchinja na kuchakata nyama kutopata mifugo bora.

Akizungumza jana katika Kijiji cha Kinango wilayani Magu Mkoani Mwanza wakati akishuhudia zoezi la uogeshaji mifugo dhidi ya magonjwa mbalimbali katiak ziara yake ya siku mbili mkoani humo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki alisema, “Nchi yetu ina ng’ombe wengi sana, lakini wengi siyo bora kama inavyotakiwa sasa tunatakiwa kutoka kuwa na ng’ombe wengi tu bali tuwe na ng’ombe walio bora.

“Tukiwa na ng’ombe wengi wasio bora hawatusaidii sana katika maisha yetu, kwa sababu lengo la kuwa na ng’ombe atupe nyama, atupe maziwa na atupe kipato sasa tufikirie kuwa na ng’ombe bora na moja ya njia ya kuwa na ng’ombe bora ni hii ya kuwaogesha,” alisisitiza Ndaki

Kwa upande wake Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Nchini (TMB) Iman Sichalwe amewaeleza wafugaji kuwa suala la kuogesha mifugo dhidi ya magonjwa ni muhimu kwa kuwa uogeshaji unaboresha afya ya mfugo ikiwemo ya nyama na ngozi hivyo kuvifanya viwanda kufanya kazi na kuwaongezea vipato wananchi kwa kupata masoko ya kuuza mifugo yao.

Chanzo: habarileo.co.tz