Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washauriwa kuanzisha ushirika wa wakulima wa ndizi

5e2ed61d0cfbc884fda9f78afb2da405 Washauriwa kuanzisha ushirika wa wakulima wa ndizi

Mon, 19 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAKULIMA wa zao la ndizi wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro wameshauriwa kuungana na kuanzisha ushirika wa zao hilo ili waweze kupata faida kubwa, kusimamia mashamba yao na kujikimu katika mahitaji ya kifamilia.

Meneja wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Kituo cha Tengeru Arusha, Dk Mpoki Shimwela alisema hayo kwenye kikao kilichowakutanisha madiwani, wakulima, wataalamu wa kilimo pamoja na watafiti kutoka TARI.

Kikao hichoi kiliitihswa ili kujadili kuanzishwa kwa ushirika ili kukabiliana na tatizo la kudorora kwa zao hilo la ndizi.

Dk Shimwela alisema uanzishwaji huo wa ushirika utasaidia wakulima kukabiliana na changamoto za soko ambalo limeshuka baada ya wakulima kulima kisasa na kupata tija kwenye zao hilo.

Shimwela alisema utafiti wa awali wa mwaka 2017 ulionesha uzalishaji wa ndizi kwa hekta kwa mwaka ni tani tisa ambapo baada ya uhamasishaji na elimu, mwaka 2020 uzalishaji umepanda hadi kufikia tani 40 kwa hekta moja.

Alisema baada ya uzalishaji huo kupanda ndizi ziliweza kuzaa kwa kilo 40 hadi 60 ingawa mkulima bado ananufaika na asilimia moja tu ya kile anachokizalisha wakati mfanyabiashara akinufaika kwa asilimia 60 hadi 70.

"Ndizi ya vichane tisa hadi 15 mfanyabiashara ananunua kwa kwa mkulima kwa Sh 3,000 huku akienda kuuza kwa Sh 30,000, hivyo ni vyema ikiwa wakulima wataungana na kuanzisha ushirika wataweza kupata faida kubwa na wataweza kusimamia mashamba yao na kujikimu katika mahitaji ya familia,"alisema.

Naye Mkulima Paul Clemence kutoka Shimbi Kati alisema wamedhamiria kuanzisha ushirika wa zao hilo ili kukabiliana na tatizo la soko hilo la ndizi.

Alisema soko la zao hilo limeshuka baada ya wakulima kuhamasishwa namna bora ya kulima kilimo chenye tija ambapo kwa sasa anaweza kupata ndizi moja yenye vichane 15 kutoka kwenye vichane sita .

Kwa upande wake, Erasmus Mkenda aliomba serikali kuwa nguzo muhimu ya kusimamia ushirika huo ili kuwasaidia wananchi kuona manufaa na kuwasaidia kulima kwa faida.

Chanzo: www.habarileo.co.tz