Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasemavyo kinamama wasiotaka kutaja baba wa watoto wao

68587 Pic+kinamama

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kinamama wametajwa kusababisha utata wakati wanapotakiwa kutoa taarifa za baba wa watoto wao kwa ajili ya utayarishaji wa vyeti vya kuzaliwa, kwa mujibu wa Wakala wa Usajili wa Vizazi na Vifo (Rita).

Wengi hufuata vyeti hivyo muda mrefu baada ya watoto wao kuzaliwa, lakini meneja mawasiliano wa Rita, Josephat Kimaro ameiambia Mwananchi kuwa kazi kubwa ni katika kupata taarifa za wazazi wenza.

Kimaro alisema mara nyingi wanakumbana na changamoto hiyo kwa kinamama wanaotafuta vyeti vya kuzaliwa vya watoto wao kwa kuwa hutaja jina la baba tofauti na lililoandikwa kwenye kadi ya kliniki.

“Kwa mfano katika taarifa zake, anataja jina la baba fulani, lakini sisi tunapoangalia kadi ya kliniki iliyopo kwenye nyaraka zetu, tunakuta jina tofauti,” alisema.

Alisema wanapoona kuna mkanganyiko huo, humuita mama mzazi ili afafanue sababu za kuweka majina ya baba tofauti.

Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi la leo Jumapili Julai 28, 2019

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz