Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasafiri wa Dar-Dodoma watakiwa kupitia Iringa

97798 Safari+pic Wasafiri wa Dar-Dodoma watakiwa kupitia Iringa

Wed, 4 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mjumbe wa Kamati ya Chama cha Wamiliki wa Mabasi  Tanzania (Taboa), Mustaphar Mwalongo ametoa ushauri kwa abiria wanaotoka Dar es Salaam kwenda Dodoma akiwataka kupanda mabasi ya Iringa kisha kuunganisha kwenda katika jiji hilo. Amesema kwa hali inavyokwenda baadhi ya mabasi yanayokwenda Dodoma yatapungua kutokana gharama kubwa ya uendeshaji wa biashara hiyo baada ya daraja la Kiyegeya kusombwa na maji jana Jumatatu Machi 2, 2020. Daraja hilo linalounganisha mikoa ya Morogoro na Dodoma lililosombwa na maji saa 9 alasiri kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa katika Mkoa wa Morogoro. Mwalongo ametoa ushauri huo leo Jumanne Machi 3, 2020 wakati akizungumza na gazeti hili kuhusu mwenendo wa hali ya usafiri wa abiria wanaotoka na kwenda mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam baada ya daraja hilo kusombwa na maji. "Mabasi yanayokwenda Dodoma yamepungua kwa haraka haraka leo asubuhi nimeona kampuni nne tu siku za kawaida kampuni zinakuwa zaidi ya 20.Sidhani kama nyingine zitaweza kwenda Dodoma kupitia Iringa maana mzunguko ni mrefu sana na gharama ni kubwa. "Ninachowashauri abiria wanaotoka Dar es Salaam ni vyema wakapanda mabasi ya Iringa kisha kuunganisha hadi Dodoma ambapo gharama yake haifiki Sh Sh 40,000," amesema Mwalongo. Kuhusu nauli kupanda, Mwalongo amesema baadhi ya mabasi yameangalia gharama ya kutoka  Dar es Salaam hadi Iringa ambayo ni Sh 22,000 na kutoka Iringa hadi Dodoma Sh 15,000 akisema bado hujaweka vibali vya kupitia njia hiyo. Amesema kwa mazingira yalivyo ni nadra kwa mabasi yanayokwenda Dodoma kuendelea na nauli ya zamani ya Sh 22,000 kutokana na hali halisi hasa kupitia njia ya Iringa. Mwalongo amesema baadhi ya mabasi yanayokwenda mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kagera, Kigoma, Singida na Tabora yamelazimika kupitia njia ya Arusha. “Naiomba Serikali irekebishe changamoto hii kwa uharaka, pia iweke mpango mkakati wa muda utakaohakikisha baadhi ya madaraja yanakuwa imara. Hizi changamo ni muda mrefu tangu Rais John Magufuli hajaingia madarakani,” amesema Mwalongo. Hata hivyo, mmoja wa (jina limehifadhiwa) wakatisha tiketi ameiambia Mwananchi  nauli za kwenda mikoa ya Kanda ya Ziwa  nauli hazijapanda na kwamba baadhi ya kampuni bado zinajitafakari kuhusu mchakato huo.

Chanzo: mwananchi.co.tz