Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Warahibu 114 wa dawa za iulevya wapewa mafunzo

A2b29b1c 5295 4e78 836e A85a7fc62a35 Warahibu 114 wa dawa za iulevya wapewa mafunzo

Sat, 3 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vijana 114 waliokuwa waathirika wa dawa za kulevya wamenufaika na mafunzo ya elimu ya ujuzi katika fani mbalimbali na kuhitimu katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi kilichopo Kibaha, Pwani.

Akitoa pongezi kwa wahitimu hao, mgeni rasmi katika mahafali hayo, Prof. Riziki Shemdoe ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI amesema;

“Nimefarijika sana kusikia kwamba kati ya wanufaika 6,157 waliosoma kwa njia ya mtandao, 114 ni ndugu zetu kutoka kundi la waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya na leo hii niko hapa kuwapa vyeti vyao ili wakaanze kufanya shughuli za kuwaingizia kipato”.

Sambamba na hilo, pia Prof. Shemdoe ameipongeza Mamlaka ya Elimu nchini (TEA) kwa kutoa ufadhili wa zaidi ya shilingi milioni 131 kwa chuo hicho ili kufanikisha mafunzo hayo kwa kipindi cha miezi mitatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live