Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanyang'anyi watiwa nguvuni Mabwepande

RPC DSM Jumanne Muliro

Fri, 24 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewakamata watu 61 wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ambapo saba kati yao yupo kijana aitwaye Yohana Zacharia maarufu kama Cobra ambapo wamekuwa wakitumia bastola bandia kutishia na kunyang'anya watu.

Taarifa hiyo imetolewa hii Desemba 23, 2021, na Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo Jumanne Muliro.

"Waliokamatwa miongoni mwao ni watuhumiwa saba, ambapo kundi hili yumo mtuhumiwa anayeitwa Yohana Zacharia maarufu kama Cobra, yeye na wenzake wamekuwa wakitumia bastola bandia kutishia watu na kunyang'anya vitu Mabwepande, Ulongoni na Banana," amesema Kamanda Muliro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live